SHULE YA UPILI YA MURURIA

MTIHANI WA KATI YA MUHULA

KIDATO CHA TATU

JINA…………………………………………………………………….NAMBARI…………………DARASA……......

 

Matumizi ya lugha


(a) (i) Toa sifa bainifu za sauti /h/ (al.2)  

 


    (ii) Unda neno lenye mpangilio huu wa silabi:KIII (ala.3)

 

 


(b) Tambua hisia zinazojitokeza katika sentensi hizi. (al 2)
     (i)Ng’oo! Mtu kama wewe huwezi kuajiriwa.

 
     (ii) Maskini! Alikuwa mpenda amani.

 

 
(c) Tunga sentensi ukitumia kiunganishi cha matokeo (al. 1)

 


(d) Changanua sentensi hii kwa michoro matawi.(al 5)
    Mwanafunzi aliyesoma kitabu jana amepita mtihani .

 

  

 

 

 

 

 

 


(e) Bainisha aina za virai katika sentensi hizi. (al.2)
       (i) Alisema atafika kesho kutwa.

 

 
     (ii) Gari lilianguka kando ya barabara.

 

 
(f) Tunga sentensi kati jinsi ya kutendesha ukitumia kitenzi ‘fa’. (al.2)

 


(g) Banisha kiima, shamirisho na chagizo katika sentenzi hii. (al 3)
      Mwanafunzi aliandika insha vizuri.

 

 
(h) (i) Akifisha kifungu kifuatacho. (al 2)
      Sijaona kitabu kizuri kama hiki utaniazima kwa siku ngapi bashiri alimsihi?

 


    (ii) Andika sentenzi ifutayo katika usemi wa taarifa (al. 2)
    “Unatwaje? Unaenda wapi? Unasoma shule gani Askari alimuuliza mwanfunzi

 

(i) Badilisha sentensi hii katika hali ya wastani (al. 1)
     Tusiyoyajua hayatuthamini.

 

 
(j) Tambulisha matumizi ya kiambishi ‘Ki’ katika sentensi ifuatayo. (al.3)

 Ukinunua zawadi na haikubaliki usijisumbue kuandika kisa hicho.

 

 

 

 
(k) (i) Tunga sentensi moja ukitumia nomino ‘ua’ kuleta maana mbili tofauti (al.2)

 

 
     (ii) Eleza maana ya vitate hivi (al.2)

      Tua


      Dua

 
(l) Andika sentensi hii upya kwa kutumia ‘amba’ (al.1)
     Basi lililogonga ng’ombe ndilo nililotaka kusafiria.

 

 
(m) Bainisha wakati katika sentensi hii. (al.1)

       Aandike


(n) Kanusha sentensi hii kwa wingi (al.1)

Tusiyalete mabata wapi? majike?

 


(o) Unda nomino mbilimbili kutokana na maneno uliyopewa (al.2)

    (i) Unga

 
    (ii) Kaa

 
(p) Tofautisha kati ya shada na kiimbo (al.2)